The House of Favourite Newspapers

Anastasia Pokreshchuk Atumia Mamilioni Kufanya Sajari Ya Mashavu

0
Ukisikia Dunia ina mambo ndiyo huku sasa! Anastasia Pokreshchuk mwenye umri wa miaka 33; ni mrembo kutoka huko Kiev nchini Ukraine ambaye amejitosa kuonesha muonekano wake wa miaka sita iliyopita alipokuwa gym kabla ya kutumia mamilioni ya pesa kufanya sajari za kututumsha mashavu.
Anastasia ambaye ni mwanamitindo maarufu ncini humo anasema alifikia hatua hiyo ili awe na muonekano ambao yeye ndiyo anaupenda kuliko wa mwanzo.
Mrembo huyo anasema kuwa, hakupenda muonekano aliokuwa nao awali ila alipotutumsha mashavu kwa sajari ndiyo anasema yuko vizuri na imemuongezea kujiamini na kuvutia madili mengi ya mitindo sehemu tofauti duniani.

Anastasia anasema wengi wanaomtafuta ni baada ya kutajwa kwenye Kitabu cha Kumbukumbu za Dunia cha Guinness kuwa ndiye mwanamke mwenye mashavu makubwa zaidi duniani.

Leave A Reply