The House of Favourite Newspapers

Angalia Pialali Alivyomtwanga Mfilipino Tinampay

0

BONDIA Iddi Pialali wa Bagamoyo Pwani hapa nchini, leo alfajili amefanikiwa kumtwanga Bondia wa Kimataifa Arnel Tinampay kutoka Ufilipino.

Tinampay alikubali kichapo hicho kwenye pambano la raundi nane lililopigwa Ukumbi wa Next Door Arena uliopo Masaki Jijini Dar.

Katika pambao hilo mabondia wote walianza kushambuliana kwa kasi kila mmoja akionekana kutaka kumlaza mwenzake kwa KO lakini kutokana na umahiri waliouonesha walijikuta wote wakimaliza raundi zote nane.

Wawili hao baada ya kumaliza pointi hizo majaji wa mpambano huo walimpa ushindi Pialali kufuatia kumtwanga ngumi Mfilipino huyo na kutaka kumuangusha mara kadhaa hali iliyopelekea aonekane kujikongoja ilimradi amalize pambano hilo.

Angalia picha

Kazi ilivyoanza.
Mtifuano.
Kuteleza si kuanguka, Pialali aliteleza ulingoni lakini aliinuka na kukaa sawa.
Tinampay akimsoma Pialali baada ya kuanza kuona mziki wake.
Pialali akipeleka konde kwa Tinampay.
Pialali akikiparaza kwa konde kichwa cha Tinampay.
Tinampay akipelekewa sumbwi.
Mashabiki midadi kama yote.
Pialali akitangazwa mshindi na mwamuzi wa pambano hilo, Pembe Ndava baada ya kumfua, Mfilipino Tinampay.
Mfilipino Tinampay akiwa haamini kilichotokea baada ya pambano kumalizika.                    HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL 
Leave A Reply