The House of Favourite Newspapers

ARIANA GRANDE AWEKA REKODI YOUTUBE KWA WIMBO, VIDEO YAKE

Staa wa muziki aina ya Pop, Ariana Grande  amevunja rekodi ya masaa 24 kwenye mtandao wa Youtube na Vevo kwa video yake ya ‘Thank You Next’.

 

Video ya Thank You Next ilitoka siku ya Ijumaa wiki iliyopita tarehe 30 na mpaka kumaliza masaa 24 ilikuwa imetazamwa mara milioni 47 huku upande wa Vevo ikifikisha watazamaji milioni 50.

 

Ariana Grande amefurahia rekodi hiyo mpya kwa kuandika kwenye mtandao wake wa Tweeter, “p.s. we set a new @vevo record. that’s wild. i love u. thank u”.

 

 

Wimbo huo aliutoa baada ya kuachana na boyfriend wake Peter Davidson ambaye ni member wa ‘SNL’(Saturday Night Live) na ulifanya vizuri sana mpaka kufanikiwa kuitoa nyimbo ya Girls Like You ya Maroon 5 katika nafasi ya kwanza kwenye nyimbo bora 100 Billboard na kuikamata nafasi hiyo kwa muda wa wiki nne mpaka wakati huu.

 

Mpaka kufikia wakati huu video ya wimbo huo tayari umeshatazamwa mara zaidi ya milioni 85. Itazame video hapo chini.

 

 Staa wa muziki wa muziki Pop, Ariana Grande  amevunja rekodi ya masaa 24 kwenye mtandao wa Youtube na Vevo kwa video yake ya ‘Thank You Next’.

Comments are closed.