The House of Favourite Newspapers

Arsenal Yainyamazisha Tottenham Hotspurs

0

ARSENALĀ  imeifunga mabao mawili ya kipindi cha kwanza na kuwalaza wapinzani wao wa jadi mjini London Tottenham kwa mara ya kwanza katika mechi saba za ligi ya Uingereza.

Beki Shkrodan Mustafi alifunga kichwa kizuri kutoka kwa krosi iliopigwa na Mesut Ozil , lakini Spurs wanadai kwamba mpira wa adhabu uliopigwa baada ya Davinson kumchezea visivyo Alexis Sanchez ulikuwa uamuzi mkali.

The Gunners waliongeza bao la pili dakika tano baadaye , baada ya mshambuliaji wa Chile Sanchez kufunga krosi iliopigwa na Alexandre Lacazzette akiwa amekaribia goli.

Sanchez alikuwa na fursa ya kuongeza bao la tatu lakini shambulio lake likapanguliwa na Hugo Lloris.

Fursa nzuri ya wageni hao ilimwangukia kiungo wa kati Christian Eriksen katika kipindi cha kwanza lakini shambulio la kimo cha paka la raia huyo wa Denmark liligonga chuma cha goli huku kipa Petr Cech akiruka na kuokoa kichwa kilichopigwa na Eric Dier.

Ushindi huo sasa umeifanya Arsenal kupanda hadi katika nafasi ya tano katika jedwali la ligi wakiwa na pointi moja juu ya kikosi cha Mauricio Pochettino.

Arsenal (3-4-2-1): Cech 6.5; Koscielny 8.5, Mustafi 9, Monreal 7.5; Bellerin 8, Ramsey 7.5, Xhaka 7, Kolasinac 7; Ozil 8 (Iwobi 84), A. Sanchez 7.5; Lacazette 7 (Coquelin 73, 6).

Unused subs: Ospina, Mertesacker, Maitland-Niles, Wilshere, Welbeck

Goals: Mustafi 37, A. Sanchez 41

Bookings: Xhaka 32, A. Sanchez 38, Mustafi 48, Monreal 73

Manager: Wenger 8

Tottenham (3-4-2-1): Lloris 6; D. Sanchez 5.5, Dier 6, Vertonghen 5; Trippier 5, Sissoko 6, Dembele 6 (Winks 62, 5), Davies 6.5 ; Eriksen 5, Dele 5 (Son 75); Kane 5 (Llorente 75)

Unused subs: Vorm, Foyth, Aurier, Walker-Peters

Booked: Kane 50

Manager: Pochettino 5

Referee: Mike Dean

*Player ratings by Adam Shergold

Leave A Reply