ARSENAL YAMALIZANA NA MABEKI DAKIKA ZA USIKU, MENEJA AMPA TANO LUIZ

ARSENAL imekamilisha dili la kuzipata saini za mabeki wawili dakika za usiku kabla ya dirisha la usajili kwa timu za Premier League kupigwa pini.

David Luiz na Kieran Tierney wamefunga pazia la usajili ndani ya kikosi hicho.

Tierney alikuwa kwenye mpango wa kikosi hicho tangu awali na amesajiliwa kwa dau la pauni milioni 30 kutoka Celtic.

Nyota wa Chelsea raia wa Brazil, David Luiz amesajiliwa kwa dau la pauni milioni 8.

Meneja wa Arsenal, Unai Emery amesema:”David ana uzoefu mkubwa na ninamuona kwa mbali akija kufanya makubwa na ninapenda kufanya naye kazi. Anajua vizuri majukumu yake ataongeza ukuta wa ulinzi,”.


Loading...

Toa comment