The House of Favourite Newspapers

Artificial Intelligence Inavyotishia Uelewa wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Kenya

0

Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, yameleta kitu kiitwacho Artificial Intelligence au kwa kifupi AI.

Hii ni teknolojia ambayo programu maalum kwenye mtandao wa intaneti, zinakuwa na uwezo wa kufanya kazi za kiakili kama binadamu na ukapata majibu papo hapo.

Miongoni mwa Open AI zinazotingisha duniani kwa sasa, ni ChatGPT, programu inayoweza kukupa majibu sahihi kuhusu karibu kila kitu unachotaka kukijua.

Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Kenya, kama zilivyo kwenye nchi nyingine nyingi, hawataki tena kuumiza vichwa vyao kusoma masomo magumu, wanachokifanya ni kutumia ChatGPT kuingiza maswali wanayoulizwa vyuoni hususan kwenye mitihani na programu hiyo inamaliza kazi, kwa ufanisi wa hali ya juu.

Jambo hilo linawaumiza vichwa wahadhiri wa vyuo vikuu ambao wana wasiwasi kwamba ndani ya miaka michache ijayo, kutakuwa na wahitimu wenye alama za juu kwenye vyeti vyao lakini ambao hawana kitu kichwani kwani walitumia ChatGPT kufaulu mitihani yao!

Yajayo yanasisimua!

KUMBE KAJALA ALIMKATAZA PAULA KUWA na MARIOO – ”ANAKUTUMIA, AMEPITA RAYVANNY, YUKO WAPI?”…

Leave A Reply