The House of Favourite Newspapers

ASIYEJULIKANA ATOWEKA NA MKE WA MTU!

Halima Kassim anayedaiwa kutoweka na mtu asiyejulikana.

DAR ES SALAAM: Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanaume mmoja, mkazi wa Kigogo jijini Dar, Ally Herry, anahaha kumtafuta mkewe, Halima Kassim anayedaiwa kutoweka na mtu asiyejulikana hivyo kulazimika kuomba msaada serikalini.

Akilisimulia Uwazi mkasa wake huo, Herry alisema kuwa, mkewe Halima alitoroshwa katika nyumba yao Februari 6, mwaka huu maeneo ya Kigogo, Dar katika mazingira ya kutatanisha.

Alisema kuwa, anamjua vizuri Halima kuwa ni binti anayependa mambo makubwa hivyo siku hiyo alipochelewa kumtimizia mahitaji yake, amani ilitoweka nyumbani kama kawaida yake na kuanza kufanya vituko.

Ally Herry.

“Siyo mara ya kwanza kwa Halima kutoweka nyumbani kwangu. Kuna kipindi aliwahi kutoweka, akarudi kwao mkoani Morogoro.

“Nilipomtafuta tulisuluhishwa, lakini akawa anadai kuwa hatuendani kiumri.

“Hata hivyo, baadaye alirudi nyumbani tukaendelea na maisha kwa amani kabisa.

“Kuna kipindi nilimnyang’anya kabisa simu kwani alikuwa anaendelea kuwasiliana na mtu wake asiyejulikana.

“Siku alipotoweka na huyo mtu wake, tulizozana kidogo tu baada ya kushindwa kumtimizia mahitaji yake fulani kwa sababu ni mjamzito, basi alinitengenezea kesi kwenye serikali ya mtaa kuwa nilimpiga na hapo ndipo akatoweka jumla,” alisema Herry.

Mwenyekiti.

 

Aliendelea kusimulia kuwa, baada ya Halima kutoweka, alianza kumtafuta kila kona ya Jiji la Dar ambapo alitoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Mburahati, Dar na kupewa jalada la kesi namba MBR/ RB/189/2018- TAARIFA.

Alisema kuwa, wakati akiendelea kumsaka mkewe, ndipo alipotokea mmoja wa ndugu wa mkewe Halima na kumwambia kuwa, asihofu na kupata tabu kumtafuta mkewe kwani alionekana maeneo ya Mtaa wa Tabata-Liwiti jijini Dar.

“Ndipo nikafunga safari hadi Tabata-Liwiti kisha nikatoa taarifa kwenye serikali ya mtaa.

“Baadaye nilioneshwa nyumba anayokaa, lakini nilipogonga, wenyewe walinitukana sana.

“Nilipoona hivyo, nilitafuta polisi ambaye walikubali, tukaingia ndani kisha tukakagua, lakini hatukumpata Halima.

“Niliendelea kuulizia kwa majirani ambao nilipowaonesha picha walisema huwa wanamuona,” alisema Herry.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Tabata Liwiti, Shina Namba Tatu, Khadija Abdallah alipoulizwa juu ya suala hilo alikuwa na haya ya kusema:

“Binafsi nimeshawahi kumuona huyo Halima mtaani kwangu, cha msingi ni yeye na mkewe kukaa na kuyamaliza maana naamini ni mambo ya kifamilia na hata waliokuwa kwenye ndoa wanajua hii ni sehemu ya mitihani tu.”

Imeandikwa na Mayasa Mariwa ta na Gladness Mallya.

 

Stori: WAANDISHI WETU

Comments are closed.