The House of Favourite Newspapers

Kauli ya Tume ya Haki za Binadamu Kuhusu Kifo cha Akwilina

Tume ya Haki za Binadamu nchini kupitia Jukwaa la Wakurugenzi wa Asasi za Kiraia (AZAK) imesema imesikitishwa na ilichokiita vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, utawala wa sheria na usalama wa raia  nchini.

 

Miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na mauaji ya mwanafunzi wa Chuo cha Taifa Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini, ambayo yameleta simanzi kwa taifa. Matukio mengine ni ya kutekwa, kuuawa, kuumizwa na kupotea kwa watu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na  kutekwa na kuuawa kikatili kwa kiongozi wa Chadema, Daniel John, mnamo Februari 11, 2018.

 

Matukio mengine ni kupigwa risasi hadharani kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kupotea kwa mwandishi wa Mwananchi, Azory Gwanda  na kupotea kwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Ben Saanane.

 

SHUHUDIA VIDEO YA TUKIO HILO

Comments are closed.