The House of Favourite Newspapers

Askofu Ashtakiwa kwa Kupapasa Titi la Mwanamke na Kujaribu Kumbusu

0

Askofu mmoja anayehusishwa na kanisa la Kianglikana jijini Nairobi ameshtakiwa kwa kumnyanyasa mwanamke mmoja kwa kumshika matiti na kujaribu kumbusu bila idhini.

Askofu Joel Waweru alishtakiwa mbele ya hakimu wa Kibera Derrick Kuto ambapo alikanusha makosa mawili yanayohusiana na unyanyasaji wa kingono ambayo yalimkabili.

Kulingana na karatasi ya mashtaka, kasisi huyo alitenda kosa hilo mnamo tarehe tofauti na nyakati tofauti katika kaunti ndogo ya Lang’ata , kaunti ya Nairobi.

Karatasi ya mashtaka iliyosomwa kortini ilisema kwamba Waweru akiwa mtu mwenye mamlaka aliendelea kumtongosa J.N.M akijua fika kuwa hatua kama hizo hazikubaliwi na J.NM.

Mshukiwa alishtakiwa kwa kosa la pili la kushika titi la J.N.M kwa njia isiyofaa mnamo Julai 13, 2021.

Kulingana na ripoti ya polisi, mshtakiwa anasemekana kumnyanyasa mwanamke huyo kingono tangu 2018.

Mahakama iliarifiwa kwamba mwanamke huyo hata alishushwa cheo katika kanisa aliyokuwa, baadaye akahamishiwa akapelekwa katika kanisa tofauti na mshahara wake ukakatwa.

Ripoti ya polisi ilisema mwanamke huyo alilalamika kwamba askofu huyo kwa nyakati tofauti alimwaibisha, na kumtaka awaambie waumini kwamba hajawahi kumwagiza washiriki ngono kama uvumi ulivyodai.

Kwa mujibu wa ripoti hizo, mwanamke huyo pia aliwaambia polisi kwamba askofu huyo pia alijaribu kumbusu lakini mkewe aliingia ofisini na hakuona chochote.

Ripoti ya polisi inaeleza zaidi kuwa siku moja akiwa na doa kwenye blauzi yake, mtumishi wa Mungu alifika ofisini mwake na kumshika matiti mahali doa lilikuwa kwa njia isiyofaa, jambo ambalo lilimfanya akose raha na utulivu.

Aliripoti kwa polisi kwamba askofu aliendelea kumwambia kwamba yeye ni mrembo na anampenda.

Ripoti ya polisi inasema kuwa, mwanamke huyo anahisi Askofu ana hisia za kimapenzi kwake ilhali ameolewa.

Inasemekana kwamba askofu huyo alimuita mbele ya wazee wa kanisa na kudanganya kuwa aliwaita “ihii” , kumaanisha wanaume ambao hawajatahiriwa.

Polisi wanasema kwamba mwanamke huyo alihisi aibu na kuchanganyikiwa kihisia na kuhisi kutokuwa salama.

Hata hivyo, askofu huyo alikana mashtaka hayo yote na kuomba apewe masharti nafuu ya dhamana.

Kuto alimwachilia kwa dhamana ya Sh50,000 pesa taslimu na kuagiza kesi hiyo itajwe baada ya wiki mbili.

Leave A Reply