The House of Favourite Newspapers

Askofu Kilaini Amsamehe Padri Aliyegombea Ubunge

0

ASKOFU Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amesema kuwa, milango iko wazi ya kurudi kundini kwa Padri Ildephonce Katundu aliyesimamishwa kutoa huduma za kipadri baada ya kujitosa kugombea Ubunge wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 

Akizungumza na Gazeti la UWAZI, Askofu Kilaini alisema kuwa, Padri Ildephonce asingepokelewa endapo kama angekwenda kuoa au kufanya kitu kingine kibaya kinachofanana na hicho.

 

“Utaratibu wa Kanisa Katoliki haumzuii Padri Ildephonce kurudi kundini, akiamua kurudi, atarudi tu, maana tunaambiwa mtu akikosea saba mara sabini, anatakiwa asamehewe, hivyo akiamua kurudi tutamsamehe na tutampokea.

 

“Maana hana shida yoyote, aliamua kuondoka mwenyewe, hatukumfukuza hivyo hana pingamizi lolote, akirudi tunampokea,” alisema Askofu Kilaini.

 

Alisema kuwa, Padri Ildephonce hakuwa na tatizo lolote, bali aliamua tu mwenyewe kufanya hicho kitu (kugombea) japokuwa alikuwa anajua kabisa havichanganyiki, lakini akaamua hivyo.

 

Askofu Kilaini alisema kuwa, muda alioandika barua na kuamua kuchukua uamuzi haukuwa unatosha “Hadi sasa hatujampata, hivyo tunamngoja tu hadi arudi maana bado muda upo kwa kuwa siku aliyochukua fomu ya kutia nia kugombea ubunge na siku ya uchaguzi wa kura za maoni, hakuna kiongozi wa Kanisa Katoliki ambaye alimuona kwani tungeweza kuongea naye.

 

“Hatukujua kama amegombea ubunge kwa sababu haturuhusiwi kuingia kwenye siasa,” alisema Askofu Kilaini.

 

Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli ameeleza kufurahishwa na mafuriko ya watu waliohudhuria katika mkutano wa kampeni za chama hicho mkoani Gazeti hili lilipomtafuta Padri Ildephonce kwa njia ya simu ili atoe ufafanuzi kuhusu uamuzi aliochukua wa kugombea ubunge wakati akijua kanuni za Kanisa Katoliki haziruhusu kufanya hivyo, alijibu kwa kifupi; “Samahani, samahani, samahani sana.”

 

Kisha akakata simu. Katika uchaguzi huo hatua ya kura za maoni ndani ya CCM, Padri Ildephonce alipata kura 0 kati ya kura zilizopigwa na wajumbe 527 kwenye jimbo hilo ambapo Florent Kyombo aliibuka kidedea.

Habari; Nyemo Malecela, KAGERA

Leave A Reply