The House of Favourite Newspapers

Askofu Malassy Kuombea Amani Taifa

0

1.Askofu Godfrey Malassy (kushoto) akizungumza jambo na kulia kwake ni, Mchungaji wa kanisa hilo, Oliva Mallonga.Askofu Godfrey Malassy (kushoto) akizungumza jambo na kulia kwake ni Mchungaji wa kanisa hilo, Oliva Mallonga.2.Mchungaji Mallonga (kulia) akionesha vitabu vinavyouzwa.Mchungaji Mallonga (kulia) akionesha vitabu vinavyouzwa.3.Wanahabri wakifuatilia hafla hiyo.Wanahabari wakifuatilia hafla hiyo.4.Askofu Malassy (kushoto) akisoma taarifa yake.Askofu Malassy (kushoto) akisoma taarifa yake.

ASKOFU wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches, Godfrey Emmanuel Malassy anatarajia kufanya maombi maalum kwa ajili ya mkesha wa kuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, lengo likiwa ni kudumisha amani ya taifa letu.

Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar, Askofu Malassy alisema mbali na kuombea amani kwa taifa, pia watatumia siku hiyo kumuombea Baraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli kwa weledi wa kazi ya kuliongoza taifa katika mstakabari mzuri.

Pia, askofu huyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba na kuwaalika Watanzania kujitokeza kwa wingi, ili kuunga mkono kongamano hilo ambalo linatarajiwa kufanyika ndani ya Uwanja wa Taifa, Temeke jijini Dar, ambapo hakutakuwa na kiingilio chochote, ili washiriki hafla hiyo muhimu kwa ajili ya taifa na watu wake.

Mbali na kongamano hilo, pia siku hiyo kutakua na kitabu alichokiandika kikielezea umuhimu wa Amani kwa taiafa, kiitwacho Ijue Siri ya Amani kwa Taifa, ambacho kipo mitaani na kupatikana kila mahali nchini, huku akiweka wazi kuwa endapo mtu atakihitaji kabla ya siku hiyo, anaweza kuwasiliana na wauazaji kupitia namba 0755202204, 0719202204 na 0684202204.

Ambapo kwa mujibu wake, mapato yatakayotokana na mauzo ya kitabu hicho yatachangia huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo kusaidia wagonjwa mahospitalini.

Aidha askofu Malassy alisema mgeni rasmi wa hafla hiyo anatarajia kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply