The House of Favourite Newspapers

Aslay Amkuna Lady Jaydee

0
Aslay Isihaka

MKONGWE katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee amefungukia kukunwa kwake na kazi za msanii mwenzake, Aslay Isihaka anazozifanya kwa sasa.

 

Akipiga stori na Risasi Vibes juzikati, Lady Jaydee alisema anapohitaji kusikiliza muziki mzuri, husikiliza muziki wa Dogo Aslay na amekuwa akiusikiliza hata kutwa nzima kwa kuwa kazi zake za sasa, zinakata kiu ya burudani anayoitaka.

Lady Jaydee

“Mimi ni mwimbaji, lakini haina maana kwamba sipati burudani kwa wenzangu, mfano huwa natumia saa nyingi, wakati mwingine nashinda kutwa nzima nasikiliza kazi za Aslay, anajua kuimba na kuandika nyimbo nzuri,” alisema Jaydee

Leave A Reply