The House of Favourite Newspapers

Chuz: Kiki Hazina Mpango

0

 

Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’

MKONGWE wa filamu za Kibongo, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ ameibuka na kuwataka wasanii wenzake kuachana na kiki kwani hazina mpango bali zinawabomoa na kuzidi kuua tasnia ya filamu.

 

Akichonga na Za Motomoto News, Chuz alisema wasanii wanatakiwa kuelewa kwamba kiki bila kufanya kazi ni bure kwani mashabiki wanachotaka ni kuona kazi zao bora na siyo kiki au skendo zisizokuwa na kichwa wala miguu.

 

“Jamani wasanii wenzangu pigeni kazi, achaneni na kiki kwani siyo mpango, niko huku Lushoto kwa miezi kadhaa sasa nafanya kazi ya tamthiliya na nimeshamaliza Closed Chapter sasa naanza nyingine mpya naamini kila msanii angekuwa kama mimi, tasnia ya filamu ingerudi kwenye ubora wake kama zamani,” alisema Chuz

Leave A Reply