The House of Favourite Newspapers

ATE YATOA TUZO KWA MWAJIRI BORA 2019

0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB) akihutubia wageni waalikwa wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali.
Mhagama (MB) akitoa tuzo kwa mwajiri bora wa mwaka 2019 Mwakilishi kutoka kampuni ya TBL David Magese wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE). Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka na Mwenyekiti wa Bodi wa chama hicho Jayne Nyimbo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Stella Ikupa (katikati), akitoa tuzo kwa mwajiri bora wa mwaka 2019 kwa nafasi ya mshindi wa pili Mwakilishi kutoka  Geita Gold Mine  Elizabeth  Karua, wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).
Mhagama (MB) akishuhudia  tuzo zikiendelea kukabidhiwa  kwa  Kaimu Mkurugenzi Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Edna Chogo (kulia), wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Leave A Reply