The House of Favourite Newspapers

Staili ya Maziwa Wazi kwa Mastaa Mmmh!

0

SIYO kila kitu ni cha kuiga, bali vingine unaviacha vipite maana vinaweza kuleta madhara, hivyo ni vyema ukapishana navyo tu kwa sababu havitakusaidia.

 

Wapo wanawake wengi wakiwemo mastaa wamejikuta katika wimbi la kuiga kila staili; iwe ni mavazi, mapambo na namna ya kuendesha maisha yao yaani wanajikuta wakiishi maisha ambayo siyo yao.

 

 

Kikubwa zaidi kinachowaharibu wanawake ni utandawazi, mambo mengi wanayaona mitandaoni na kutaka kujaribu kila wanachokiona ambapo vingine unakuta ni kinyume na maadili ya Mtanzania.

 

Kwa sasa mastaa wengi wameibukia kwenye staili ya suti za vifua wazi ambapo licha ya kwamba wanapendeza lakini kwa upande mwingine siyo sawa kwani wakati mwingine hujikuta sehemu yote ya kifua ikibaki nje na kila wakati kuwa na kazi ya kuweka nguo vizuri.

 

Hivi karibuni staa wa fi lamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliweka picha akiwa amevaa suti ambayo ilimwacha wazi sehemu kubwa ya kifua huku sehemu ya mapaja nayo ikiwa wazi.

 

Kutokana na picha hiyo kusambaa katika mtandao wa Instagram, mchumba wake, Majizzo aliandika maneno na kumwambia wengine pia ambao wameachia picha za aina hiyo kwani inakuwa ni kama wanaigana akiwemo, Faustina Charles ‘Nandy’, dada wa Mbongo Fleva; Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Khan, mke wa mwanamuziki, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Fahyma.

 

 

Staili hii siyo sawa kwa maadili ya Kitanzania kwani kifua cha mwanamke ni sehemu nyeti ambayo inatakiwa kuheshimiwa na kusitiriwa sana pamoja na sehemu ya mapaja.

 

Lakini mastaa wengi au wanawake wengi wa siku hizi wameona ndiyo sehemu za kuacha wazi siku hizi, sijui wanafaidika na nini na sababu za wao kufanya hivi ni nini.

 

 

Wanawake mnatakiwa mjitambue, mjipende, mjiheshimu na ndipo mtaheshimiwa, heshima ya mwanamke inashuka hivi sasa kutokana na wengi kujiweka hovyo kwa kuiga tamaduni nyingine ambazo siyo zao.

 

Ni vyema mjitathimini, kuwa staa siyo lazima kukaa nusu utupu, tambueni kuwa nyie ni kioo cha jamii na siyo kila staili ya nguo ni ya kuvaa, nyingine ziacheni ziwapite tu.

Makala: Gladness Mallya

 

MAMA ALIYEACHA KAZI KWA LUGOLA, ILI KUOMBEA WATU – “ANA DEGREE 2”

Leave A Reply