The House of Favourite Newspapers

Atembea na Mtoto wa Shehe, Nyeti Zake Zatoweka Kimaajabu

MSHTAKIWA Faraji Ramadhani mwenye umri wa miaka 27 ameiomba  Mahakama ya Mwanzo Jijini Mbeya imruhusu ajidhamini mwenyewe kutokana na sehemu zake za siri kutoweka hivyo kupata maumivu makali anapokuwa mahabusu.

 

“Hakimu nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa shehe, Ustadhi huyo alinionya sana kuachana na binti yake lakini sikusikia, ndio chanzo cha sehemu zangu za siri kupotea, nikiwa nyumbani natumia dawa za miti shamha kutuliza maumivu,” alisema Ramadhani mahakamani.

 

Kutokana na malalamiko hayo Hakimu Manase aliamuru mtuhumiwa huyo aliyefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la wizi wa kompyuta akaguliwe na baada ya askari kumkagua ilibainika anachokisema ni kweli.

 

Hata hivyo,  Hakimu Diana Manase wa Mahakama hiyo ya Mwanzo Jijini Mbeya aligoma kumruhusu kujidhamini kwa madai akitoroka hawezi kujua wapi kwa kumpata na kumtaka avumilie kwa kuwa tatizo kalitafuta mwenyewe maana shehe alimuonya aachane na binti yake akakaidi,

Kesi imeahirishwa hadi Septemba 27 mwaka huu.

Comments are closed.