The House of Favourite Newspapers

Vodacom yatoa TZS bilioni 54.5 kama gawio kwa wanahisa

  • Vodacom yatoa taarifa ya ongezeko la faida kwa mwaka kufikia TZS billioni 90.2

Tarehe 20 Septemba 2019 – Dar es Salaam

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania, Vodacom Tanzania PLC imetangaza faida ya mwisho wa mwaka ya kiasi cha TZS bilioni 90.2 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ulioishia mwezi Machi mwaka huu.

Wakati huohuo Kampuni ya Vodacom ambayo ina mtandao wenye kasi zaidi nchini inajivunia thamani iliyojitengenezea katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni ikiwemo TZS bilioni 54.5 ambazo zimelipwa kama gawio kwa wanahisa.

Ongezeko hili limechangiwa na kuongezeka kwa mapato yatokanayo na huduma ambayo yanafikia TZS bilioni 1018.9, ambayo yamesababishwa na kukua na kuimarika kwa mapato yatokanayo na huduma za M-pesa, ununuzi wa Intaneti (Bando) na mapato yatokanayo na ujumbe wa simu. Kampuni ya Vodacom imepata wateja wapya wapatao milioni 1.2 katika mwaka huuwa fedha jambo ambalo linaongeza idadi yake ya wateja kufikia milioni 14.1.

Katika mwaka huu wa fedha kampuni ya Vodacom ilifanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya TZS bilioni 171.4 sawana (asilimia 16.7% ya mapato) katika kupanua mtandao wake, kuongeza maeneo yanayopata mtandao wa 4G katika miji mikubwa nchini, kuongeza uwezo na kuboresha mtandao kuweza kutoa huduma ya data ya kiwango cha juu kwa wateja.

Wakati huo Shilingi bilioni 59 zimewekezwa katika mishahara, mafunzo na maendeleo ya wafanyakazi wake wa kudumu wapatao 548 pamoja na kutoa ajira isiyo ya moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 127,000.

Akiongea katika mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni ya Vodacom leo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom bwana Ali A. Mufuruki amesema, “Kampuni ya Vodacom vilevile inajivunia uwekezaji wake katika jamii ambao unathama ni ya jumla ya shilingi trilioni 1.1, ambazo ni fedha zilizochangiwa katika uwezeshaji wa jamii kupitia kodi, ada za udhibiti katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ambapo malipo ya zaidi ya Shilingi trilioni 0.4 yalifanyika katika mwaka 2019 peke yake.”

“Ukuaji katika sekta ya mawasiliano imekuwa wa pole pole katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Tukiwa kama watendaji muhimu katika sekta hii, tunajivunia katika ukuaji wa sekta hii,” alihitimisha Mfuruki.

Mwisho.

Kuhusu Vodacom: Vodacom Tanzania PLC ni watoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi wanaoongoza wenye mtandao wa data wenye kasi zaidi nchini. Tunatoa huduma za mawasiliano kwa zaidi ya wateja milioni 14.

Kampuni ya Vodacom Tanzania pamoja na kampuni zake tanzu ni sehemu ya kundi la makampuni ya Vodacom (Vodacom Group) iliyosajiliwa Afrika Kusini ambayo kwa upande mwingine inamilikiwa na kundi la makampuni la Vodacom Plc la Uingereza. Kampuni ya Vodacom imesajiliwa katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kwanamba ISIN: TZ1886102715 Stock name: VODA.

Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea tovuti yetu: www.vodacom.co.tz

Comments are closed.