The House of Favourite Newspapers

Atletico Madrid ‘yamfukuza’ Diego Costa

Diego Costa

KLABU ya Atletico Madrid ipo tayari kumuuza straika wake, Diego Costa kutokana na utovu wa nidhamu lakini kocha wake, Diego Simeone anataka abaki.

 

Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Atletico wamechoshwa na tabia zake ambazo zimekuwa zikiigharimu timu huku uwezo wake uwanjani ukiwa hauridhishi pia.

 

Msimu wa Costa kwa sasa umeshamalizika kwa kuwa amefungiwa kutocheza mechi nane kutokana na kumtukana mwamuzi katika mchezo dhidi ya Barcelona, mapema mwezi huu. Upande wa Simeone ameshikilia msimamo wake kuwa bado anamuhitaji mchezaji huyo licha ya kuwa amekuwa na matatizo kadhaa.

 

Costa alimtolea lugha kali mwamuzi, Gil Manzano huku akimshika na kumtikisa kwenye mikono, baada ya kupewa kadi nyekundu na timu yake ilifungwa mabao 2-0. Simeone hakumtetea Costa kwa kile alichokifanya lakini bado anaona ni mchezaji sahihi kuendelea kubaki kikosini hapo.

 

Hii ni mara ya pili Costa anaitumikia timu hiyo, awali aliondoka kwenda Chelsea lakini akarejea klabuni hapo kwa ada ya pauni 53m mwaka 2017. Amefunga mabao matano katika mechi 21 za michuano yote alizocheza.

Comments are closed.