The House of Favourite Newspapers

ATM ya Maziwa Yazinduliwa Moshi

HAKIKA Teknolojia inazidi kukua nchini Tanzania, leo Alhamisi, Oktoba 3, 2019 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira amezindua ATM ya kwanza ya kuuza maziwa katika Mtaa wa Chagga, Kata ya Kiusa, Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Mradi huu umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya na Kusimamiwa na SNV pamoja na Match Maker Associates ambapo wameweza kujenga ATM 3 za kuuza Maziwa.

ATM zingine zipo Wilaya ya Hai na nyingine Mjini Arusha. Sambamba na zoezi hili, Mhe Mkuu wa Mkoa amezindua Jukwaa la Ubunifu la Maziwa Mkoa wa Kilimanjaro ambapo amekubali kuwa mlezi wa Jukwaa hilo.

 

 

Comments are closed.