The House of Favourite Newspapers

Aunt: Acheni Kuita Wapenzi Wa Wenzenu Wadogo

0

Ukitaja mmoja wa wasanii walioweza kuifanya Bongo Muvi kusonga mbele, kamwe huwezi kuacha kulitaja jina la mwamama mrembo, Aunt Ezekiel kwa sababu ni mmoja wa wasanii wa kike  watano walioweza kujizolea umaarufu mkubwa sana kupitia tasnia hiyo.

 

Msanii huyo amezungumza vitu vingi sana kupitia Showbiz Xtra na ameweza kufunguka vitu vingi vinavyomhusu:

Showbiz: Habari mama Cookie?

Aunt: Salama kabisa, haya kuna jipya tena.

Showbiz: Hakuna jipya lakini wasomaji wanataka kufahamu kama mama kijacho unaendeleaje na bado hujaamua kumuweka wazi baba kijacho.

Aunt: Cha kushangaza sana kwa nini watu wanapenda kujua baba kijacho wa wenzao kwa sababu mwisho wa siku lazima ujauzito uwe na baba yake.

 

Showbiz: Ni sababu ipi iliyokufanya kuficha ujauzito wako mpaka dakika za mwisho?

Aunt: Kila kitu ni uamuzi tu, ni jambo ambalo ni niliamua mwenyewe kabisa kwa ajili ya mipango yangu.

 

Showbiz: Watu wengi wanashangazwa na kitendo cha wewe kuachana na Mose kwa muda mfupi na ukapata ujauzito, wengi wao wanadai itakuwa ujauzito ni wa Mose kuna ukweli katika hilo?

Aunt: Sasa wenye kujua kabisa siku mpaka mimba inaingia, wanasema ni ya Mose, sasa ni bora tu niwaachie wao maana wao ni hakimu wa kila kitu.

 

Showbiz: Inadaiwa sasa hivi uko kimapenzi na Kusah na Kusah alikuwa mpenzi wa Rubby, hiyo inakuwaje hapo.

Aunt: Nilishawahi kusema, hakuna mapenzi ya siri hata siku moja. Kwa hiyo, kama ni mpenzi wangu, basi itajulikana tu.

Showbiz: Ukiangalia kwenye mitandao ya kijamii, wanazungumzia umri ambao Kusah anao ni tofauti kabisa, kwamba wewe mkubwa yeye mdogo, unazungumziaje hilo?

 

Aunt: Kinachoshangaza kwa nini wanapenda kuwaita watoto wa wenzao wadogo, kivipi sasa! Mtu akiwa kwenye uhusiano tu utasikia mdogo, hebu waache hiyo tabia. Mtoto mdogo hawezi kuingia kwenye uhusiano hata kidogo.

 

Showbiz: Ila kuna tetesi kuwa Mose Iyobo ndiyo kiboko yako, hivyo hata baada ya kujifungua mtarudiana.

Aunt: Nafikiri wao ni watabiri wakubwa, haya ngoja tuone wanavyosema wao, maana wanajua kila kitu kuliko mimi mwenyewe.

Showbiz: Mose anakuja kumuona mtoto wake na kutoa matumizi mengine kama baba?

Aunt: Ninachojua Cookie, Mose ni baba yake, mengine tuendelee kumuomba Mungu.

Showbiz: Mtu ambaye mko naye kwenye uhusiano hivi sasa, anamchukuliaje mwanao Cookie?

Aunt: Anampenda na kumjali, anawezaje sasa kutompenda mtoto wangu halafu na mimi nipo tu.

 

Showbiz: Vipi kuhusu bifu lako na Shamsa limeishaje?

Aunt: Mimi kwa upande wangu liko palepale.

Showbiz: Mbona kama mlianza kuwa pamoja na mlikuwa mnatumiana ujumbe kwenye posti zenu za Instagram kana kwamba mmeshamaliza bifu lenu.

Aunt: Shida ya watu wengi, mitandao ya kijamii ndiyo imekuwa kila kitu kwao.

Showbiz: Mitandao ya kijamii imekuathiri kwa kiasi gani.

 

Aunt: Mitandao ya kijamii ina athari zake kubwa tu na imeshawahi kuniletea shida, lakini mwisho wa siku inasaidia kwa upande mwingine kwa ajili ya kujitangaza.

Showbiz: Ushoga wa Kajala na Wema, umerudi na Wewe Wema alikuwa ni rafiki yako sana, vipi unawezaje kuendesha urafiki wenu mkiwa watatu?

 

Aunt: Kwani urafiki ni lazima uambatane na mtu kila wakati, kwa upande wangu mimi nafurahia sana tu, walivyopatana, tutaendelea kuwa marafiki wote kwa sababu tunajuana vizuri.

 

Showbiz: Kwa upande wako Cookie, unamchukuliaje licha ya kwamba ni mwanao?

Aunt: Cookie kwanza ni rafiki yangu mkubwa sana, kingine ni mwalimu wangu.

Showbiz: Ukisema mwalimu wako, unamaanisha nini?

 

Aunt: Unajua mtoto wangu kuna wakati anapenda wote tuzungumze lugha ya Kiingereza, kwa hiyo namwambiaga sijui anacheka kisha anaanza kunifundisha.

Showbiz: Mara nyingi wewe ni mtu wa kusafiri huko na kule, vipi kwa upande wa Cookie inakuwaje?

Aunt: Ninapoondoka lazima najua nimemuacha na mtu ambaye anaeleweka na hata nikirudi mtoto wangu anakuwa sawa tu.

 

Showbiz: Najua hivi sasa hauishi na baba yake lakini toka huko nyuma alionyesha wazi mtoto anampenda sana baba yake, hii hali inakuwaje kwa sasa ambapo hampo pamoja?

Aunt: Kuna vitu fulani vinapotokea, huwezi kuvizuia ila kama baba yake anamuona kila siku kwa maana anampeleka shule na kumrudisha, ingawa atagundua kuna utofauti.

 

Showbiz: Kitu gani unachokiona kwa Cookie kila anapoishi naye na jinsi anavyokua.

Aunt: Kwanza kabisa ni mtoto anayenipenda sana na kingine atakuja kuwa mtu mwenye upendo wa hali ya juu na kila siku namuombea kwa Mungu akue katika hilo.

 

Showbiz: Unawezaje kwa sasa kuwa peke yako bila baba yake?

Aunt: Yaani huelewi tu, Cookie ndiyo taa yangu, anapokuwepo yeye kila kitu kipo sawa tu.

Showbiz: Hauna mpango wa kuzaa mtoto mwingine?

 

Aunt: Kwa sasa sina ratiba hiyo kwenye kichwa changu.

Showbiz: Watu wengi kwenye mtandao wanalaumu kumsuka mtoto nywele za watu wazima, unazungumziaje?

Aunt: Unajua yule ni mtoto wangu, nina maamuzi yangu maana hao mama wa mitandao wamenichosha.

Showbiz: Asante sana.

Aunt: Karibu!

Na Imelda Mtema

UTACHEKA! VITUKO vya RIYAMA ALLY, ASHA BOKO kwenye BIRTHDAY ya LUCKYNESS MOKIWA….

Leave A Reply