The House of Favourite Newspapers

Aunt Hataki Tena Kuisikia Ndoa!

WAKATI ikiaminika wanawake wengi huitamani ndoa kwa gharama yoyote, staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel yeye hataki kusikia tena mambo ya ndoa, anasaka fedha na mpenzi wake wa sasa. 

Akizungumza na Amani, Aunt alisema suala la kutotaka ndoa si lake peke yake kwani hata mpenzi wake wa sasa Alfa halihusudu.

 

“Mimi sina ujinga wa kuolewa tena sasa hivi maana ungekuwa unaolewa unapewa majumba na magari ningesema kuna faida lakini kuvaa shela tu na kuvua sitaki ujinga huo, sasa hivi mimi kusaka pesa tu,” alisema Aunt ambaye aliwahi kuolewa na kuishi kwa muda mrefu na wanaume tofauti kisha kuachana nao.

Comments are closed.