The House of Favourite Newspapers

Aunt: Kusah Siyo Mpenzi Wangu, ni Kaka Yangu

0


KUMEKUWA na wimbi la mastaa mbalimbali hapa Bongo kutodumu na wapenzi au waume wao na kutaka kama kuhalalisha suala la kumwagana.

 

Aunt Ezekiel ni mmoja wa mastaa wa “tupendane, tumwagane” na hii ameianza tangu mumewe wa kwanza Sunday Dimonte, kufungwa jela kwa skendo ya madawa ya kulevya.

 

Leo hii staa huyo amefunguka mengi, kuhusiana na maisha yake ya kimapenzi na jinsi anavyoishi kwa sasa na mtoto aliyezaa na mnenguaji Mose Iyobo aitwaye Cookie.

Amani: Habari yako mama Cookie?

Aunt: Salama kabisa, Global wanasemaje?

Amani: Tupo salama, ila siku hizi umekuwa adimu sana.

 

Aunt: Nipo; si unajua siku hizi tuna kazi mbili; ujasiriamali na uigizaji, hivyo muda unakuwa mchache na mambo mengi Amani: Naona unakula maisha ya usingo kwa sasa!

 

Aunt: Kabisa, sina stress; pamoja na yote, lazima maisha yaendelee.

 

Amani: Nilikuwa najua kuwa umerudisha majeshi kwa Iyobo, kimyakimya maana mastaa hamchelewi kuwasapraiz mashabiki wenu.

 

Aunt: Hapana, sisi tumebaki kuwa wazazi na si kitu kingine kabisa.

 

Amani: Mmh hujammiss Iyobo kweli? Maana mmekuwa pamoja muda na mmezaa mtoto.

 

Aunt: Hapana.

 

Amani: Sasa kuna hizi habari za kwamba, sasa hivi unatoka na mwanamuziki Kusah ambaye ni mzazi mwenziye na Rubby, ni ukweli?

Aunt: Kusah siyo mpenzi wangu, kila siku nasema nampa sapoti kwenye muziki wake, yaani tumechukuliana kama kaka na dada.Amani: Ndiyo muishi nyumba moja na inasemekana ndiyo mwenye huo ujauzito?

 

Aunt: Makubwa, kama dada anaweza kubeba ujauzito wa kaka yake, yatakuwa maajabu.

Amani: Tangu muachane na Mose Iyobo, mmeshawahi kukutana au amewahi kumuona mtoto?Aunt: Nimemuona mara moja kwenye msiba wa mke wa Babu Tale.

 

Kuhusu kuja nyumbani kumuona mtoto, hajawahi.Amani: Vipi kuhusiana na matumizi ya mtoto analeta au ndiyo unalea mwenyewe?

 

Aunt: Cookie ni mtoto wetu sote, sijamkataza kumuhudumia, ila naona kwa sasa hajajipanga.Amani: Ila inawezekana hawezi kuja hapo nyumbani kwa sababu inadaiwa Kusah yupo hapo?

 

Aunt: Hakuna kitu kama hicho, hayo ni maneno ya watu.

Amani: Sasa Cookie, anapokuuliza kuhusu baba yake huwa unamjibuje na ikizingatiwa alikuwa ni rafi ki mkubwa wa baba yake?

 

Aunt: Cookie ni mtoto, ila ana akili sana. Yeye mwenyewe akiangalia anajua tu kuna vitu haviko sawa.Amani: Unamsaidiaje hivyo unavyoviita vitu haviko sawa avione viko sawa kama watoto wengine?

 

Aunt: Kwanza naweza kusema ameanza kuzoea hali hii; halafu na mimi mama yake namfanya awe rafi ki yangu mkubwa.

 

Amani: Kuna siku nilikusikia ukisema Cookie ni mwalimu wako; sikuelewa unamaanisha nini, unaweza kunifafanulia kidogo?

 

Aunt: Unajua mtoto wangu kuna wakati anapenda wote tuzungumze lugha ya Kiingereza, nikimwambia mimi sijui ananicheka sana halafu anaanza kunifundisha na huwezi amini kwa sehemu namuelewa ndiyo maana huwa nasema ni mwalimu wangu.

 

Amani: Mara nyingi huwa unasafi ri huko na kule, vipi kwa upande wa Cookie inakuaje ukiwa haupo na ikizingatiwa hivi sasa hauko na baba yake? Nani hubaki akimuangalia?

 

Aunt: Nikiondoka huwa namuacha kwa mtu anayeeleweka na huwa hakuna shida inayotokea.Amani: Karibu miaka saba itatimu tangu mume wako Sunday afungwe, una mawasiliano naye yoyote?

 

Aunt: Hapana kwa sasa sina mawasiliano naye kama zamani, ila naamini atakuwa salama; maana hata mimi nina muda mrefu sijasafi ri kwenda Dubai huwenda ningekuwa na taarifa zake kwa kina.

 

Amani: Vipi kuhusu bifu lako na Wema Sepetu limeisha?

 

Aunt: Sisi ugomvi wetu tunamalizaga wenyewe; huwa tunagombana wenyewe na tunapatana wenyewe, watu watatuona tu tupo pamoja tena.

Amani: Nakushuru sana Aunt kwa muda wako.

Aunt: Asante sana.

STORI NA IMELDA MTEMA | GPL

Leave A Reply