The House of Favourite Newspapers

Avaa Nyoka Kama Barakoa Kujikinga na Corona

0

MSAFIRI mmoja amezua taharuki baada ya kuvaa ‘barakoa’ ya nyoka aliyokuwa amejizungushia katika shingo yake na mdomoni ambapo alionekana katika basi lililokuwa likitokea Swinton kuelekea mji wa Manchester nchini Uingereza hivi karibuni.

 

Mamlaka ya usafiri wa leri ya Greater Manchester imesema kuwa nyoka hakubaliki kufunika uso kama barakoa.

 

Abiria mmoja alisema anadhani abiria huyo alikuwa amevaa barakoa ya kisasa tu mpaka alipomuona nyoka huyo akiteleza katika chuma cha kushikia mikono.

Mkuu wa usafirishaji wa Manchester amethibitisha kuwa alikuwa ni nyoka na si barakoa halisi. Shuhuda wa tukio hilo, ambaye alitaka kutofahamika alisema, ameona kuwa tukio hilo lilikuwa la kuchekesha na kustaajabisha, aliongeza kusema kuwa nyoka huyo hakuwasumbua abiria wenzake.

 

Msemaji wa usafiri wa Manchester alisema: “Muongozo uliotolewa na serikali umesema wazi kabisa kuwa barakoa zinazoruhusiwa si lazima zile za upasuaji bali abiria anaweza kutengeneza barakoa yake anayoridhika nayo na kuivaa akiwa huru.

 

“Ingawa kuna kiwango kidogo tu cha tafsiri kwamba inaweza kumaanisha hili, hatuamini maagizo hayo yalifikia kiwango cha mpaka kuruhusu ngozi ya nyoka-hususan wakati imeambatana na nyoka.”

 

Leave A Reply