The House of Favourite Newspapers

Azam yacheza na ‘timu mbili’ kwa dakika 90

Na Omary Mdose | CHAMPIONI

DAR ES SALAAM: SHERIA ya kuwa na uwezo wa kuwachezesha wachezaji wako wote waliopo kikosini kwenye mechi moja ya kirafiki, juzi Jumatano ilitumiwa vilivyo na timu ya Mamelodi Sundowns ilipopambana na Azam katika Uwanja wa Taifa, Dar.

Mchezo huo uliomalizika kwa suluhu, Mamelodi iliweza kuwatumia wachezaji wake wote 22 waliokuwa kwenye benchi na kuifanya Azam kama vile kupambana na timu mbili kwa dakika 90.

Licha ya Azam kupambana na ‘timu mbili’ lakini walionyesha ukomavu wa hali ya juu wa kulinda nyavu zao zisitikiswe mpaka mchezo huo unamalizika.

Pitso Mosimane ambaye ndiye kocha mkuu wa Mamelodi, alifikia uamuzi huo dakika ya 70 kwa kuwatoa wachezaji wote walioanza kasoro mmoja tu ambaye ni Leonardo Castro na kuwaingiza wengine waliokuwa benchi.

Awali kabla ya hapo, kocha huyo alifanya mabadiliko kwa kumtoa kipa, Wyne Sandilands na kumuingia Kennedy Mweene muda mfupi kabla ya kuanza kwa kipindi cha pili.

Wachezaji waliotolewa dakika ya 70 ni Wyne Arendse, Anele Ngcongca, Anthony Laffor, Ricardo Nascimento, Percy Tau, Tebogo Langerman, Lucky Mohoni, Hiompho Kekana na Sibusiso Vilakazi.

Walioingia ni Asavela Mbekile, Bangaly Soumahoro, Thabo Nthethe, Siyanda Zwane, Tiyani Mabunda, Teko Modise, Mzikayise Mashaba, Thapelo Moreno, Yannick Zakri.

Azam yenyewe iliwatoa Abdallah Masoud, Yahaya Mohammed, Frank Domayo, Shaban Idd na Joseph Mahundi, nafasi zao zikachukuliwa na Samuel Afful, Mudathir Yahaya, Ennock Agyei, Abdallah Heri na Ramadhan Singano.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.