The House of Favourite Newspapers

Waamuzi wampa ajira Haji Manara

Haji Manara (kushoto) akisalimiana na Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula. Katikati ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Saleh Ally.

Na Khadija Mngwai | CHAMPIONI

DAR ES SALAAM: CHAMA cha Waamuzi Tanzania (Frat) kimetoa ‘ajira’ ya kusaka mwamuzi atakayeweza kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga kiufasaha kwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.

Uamuzi huo unakuja baada ya Manara kunukuliwa mara kadhaa akilaumu maamuzi ya waamuzi wakati wa mchezo wa timu yao na wapinzani wao wa jadi, hivyo kuelekea mechi yao ya Februari 25, mwaka huu, wameamua kumpa ajira hiyo isiyo rasmi.

Simba na Yanga, zinatarajia kukutana katika Ligi Kuu Bara ambapo awali ilipangwa wacheze Februari 18 lakini mchezo huo umesogezwa mbele kutokana na majukumu ya kimataifa ya Yanga.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwenyekiti wa Frat, Mwalimu Nassor, alisema bado hawajapanga ratiba ya mwamuzi wa mechi ya watani.

“Ni vema Manara akatafuta mwamuzi anayeona anafaa kuchezesha mechi hiyo. Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunafanikiwa kumaliza ligi salama pasipo na malalamiko kwa kuondoa malalamiko madogomadogo yatakayojitokeza na mwamuzi atakayefanya vibaya hatutamsamehe,” alisema Mwalimu.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.