The House of Favourite Newspapers

Azam Yamalizana na Jembe la Kazi Kutoka Mbao FC

0

UONGOZI wa Azam FC ume-malizana na beki wa kushoto, Emmanuel Charles baada ya kufuzu vipimo vya afya jana mchana kabla ya kupewa mkataba wa miaka miwili ndani ya klabu hiyo akitokea Mbao FC.

 

Azam FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, kwa sasa inaboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21 baada ya kuboronga msimu wa 2019/20 kwa kushindwa kutwaa taji lolote.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofi sa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit, alisema bado wana mpango wa kuendelea kuiboresha timu yao kwa ajili ya msimu ujao.

“Tumeona kipaji chake, ni kijana mdogo ambaye alikuwa Mbao FC na mkataba wake umeisha, hivyo tumemchukua akiwa huru na kumpa dili la miaka miwili ndani ya Azam FC.“Imani yetu ni kwamba atakomaa na kuwa bora kwa kuwa anakutana na wachezaji wenye uzoefu na wapambanaji,” alisema.

Wachezaji wen-gine wapya waliosa-jiliwa na Azam kwa ajili ya msimu ujao ni Awesu Awesu kutoka Kagera Sugar, Ally Niy-onzima (Rayon Sports ya Rwanda), David Kisu (Gor Mahia ya Kenya), Ayoub Lyanga (Coastal) na Ismail Aziz (Pris-ons).

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply