The House of Favourite Newspapers

Shilole: Uchebe Amenidunda Mara 26, Mpaka Mbwa Akaamka

0

STAA wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ au ‘Shishibaby’ ameamua kuvunja ukimya na kufunguka alivyokuwa akipigwa na kunyanyaswa na aliyekuwa mume wake, Uchebe.

 

Shilole ameanika hayo jana Jumatano, Agosti 12, 2020, usiku wakati akifanya mahojiano na Clouds TV kuzungumzia maisha yake na namna alivyopambana mpaka kufika hapo alipo leo.

 

“Kupigwa na wanaume sijaanza leo, tangu mwanaume wa kwanza aliyenioa nikiwa na umri wa miaka 18 alikuwa ananinyanyasa na kunipiga sana, ila kipindi hiki cha Uchebe imekuwa ‘too much’. Haya yote nilikuwa sisemi kwa sababu nilikuwa namtunzia heshima mume wangu.

 

“Uchebe amenipiga mara 26, tangu anioe, siku ya kwanza nilikuwa na-shoot na akina Soud Brown na Qwisa, akaona tumechelewa kuondoka akachukia, akachukua pikipiki akaacha gari, akaondoka kwenda nyumbani, nilipoona ameondoka nakarudi na mimi nyumbani nilipofika tu akanipokea kwa makofi, niliumia sana lakini nikamsamehe.

 

“Siku nyingine amepigiga nimechelewa kurudi kutoka kwenye msiba wa marehemu Ruge, nilipofika getini tu akanipokea kwa kipigo, nilipigwa mpaka mbwa akaamka. Siku nyingine alikuta nimekaa hapa ShishiFood na wateja, sijui alidhani ni wanaume zangu? Mimi hapa wateja ni wengi, wa kiume na wa kike, niliitwa nikachezea kipigo huko, akanimwagia chillisauce akaondoka, nikabaki nahangaika kujifuta zinawasha uso mzima.

 

“Mara ya mwisho nakumbuka Julai 6, mwaka huu, nikiwa Sabasaba nahangaika kwa ajili ya familia yangu na yeye nikampigia simu nikamuuliza mume wangu kuna habari nimesikia kuna dada umezaa nae yuko Africana sijui Africa Sana, akanijibu ndio nimezaa nae, wewe si hutaki kuzaa na mimi? Niliingia kwenye gari nikalia sana.

 

“Nilipomaliza biashara yangu nikarudi hapa ShishiFood, nikaingia ndani nikamkuta anacheza playstation, nikamsalimia Asalaam Aleykum mume wangu, hakuitikia yuko busy anacheza playstation tena ambayo nimemnunulia mimi Dubai, hadi mara mbili namsalimia hajibu, nikaingia VIP nikalala zangu.

 

“Niliamshwa na ngumi ya sikio, sijakaa sawa nikapigwa ngumi nyingine ya sikio, mara ngumi ya mbavu, nikatapika. Anasema haya niulize hapa ulichokua unauliza kwenye simu, kwa kweli nilishindwa nikamuuliza kwa nini unanipiga hivi, kosa langu kukuuliza?

 

“Unanidharirisha mbele ya watoto wangu, akasema hao ni watoto wako si wa kwangu, nilichukia hapo hapo nikasema mwanaume ambaye namhudumia kila kitu anashindwa kujali hata watoto wangu, hafai nikaapa simhitaji tena maishani mwangu,” amesema Shilole.

 

Aidha, Shilole amewataka wanawake kutokaa kimya endapo wanateswa majumbani na waume zao kama ilivyokuwa kwake, badala yake waungane wapaze sauti kukomesha ukatiri wa namna hiyo.

 

Leave A Reply