The House of Favourite Newspapers

Baada ya Koffi, Bella kutoka na Ferre

0

BELAChristian Bella ‘Obama’.

Stori: Boniphace Ngumije 

HII VIPI UNAYO! KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ hivi karibuni amefunguka kuwa, baada ya kutoka na kolabo ya Acha Kabisa aliyomshirikisha mkongwe Koffi Olomide, anatarajia kufanya kolabo nyingine na msanii mwingine kutoka Congo (DRC), Ferre Gola.

Akichonga na Uwazi Showbiz, Bella alisema anamkubali sana Ferre aliyemfanya aingie kwenye muziki na kuongeza kuwa alipoanza harakati za muziki alikuwa akikariri nyimbo za msanii huyo.

“Ferre ni msanii ambaye ameishi kwenye ndoto zangu kwa muda mrefu kwa hiyo baada ya kufanya poa na ngoma niliyopiga na Koffi, sasa akili yote kwake. Natarajia kutimiza ndoto zangu muda si mrefu mambo yakienda sawa,” alisema Bella.

Leave A Reply