The House of Favourite Newspapers

Baada ya kuachika mara 3 Dida ndoa ya 4!

0

IMG-20151220-WA0017Dida na mchumba wake wa sasa.

Na Imelda Mtema
Mtangazaji wa Radio Times FM ya jijini Dar es Salaam, Khadija Shaibu ‘Dida’ anatarajiwa kufunga pingu za maisha siku chache zijazo na mwanaume ambaye mwenyewe hakupenda kumtaja jina, hii ikiwa ni mara yake ya nne kufunga ndoa.

IMG-20151220-WA00161

Khadija Shaibu ‘Dida’ akiwa na pete ya uchumba aliyovishwa.

Akizungumza na mwandishi wetu muda mfupi baada ya kuvalishwa pete ya uchumba, Dida anayetangaza Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, alisema kwa mwanamke kuolewa ni bahati, hivyo anajihesabu kuwa miongoni mwa wanawake waliojaliwa kuwa na kismati.

Dida na GDida akiwa na aliyekuwa mumewe Gervas Mbwiga ‘G’.

“Unajua kuna watu wanaweza kusema kuwa mimi naolewa hovyo lakini hawajui siku zote kuolewa ni bahati jamani, kama mtu huna hiyo bahati unawezaje sasa kupata mume? Haiwezekani kabisa,” alisema Dida na kuongeza kuwa siku zote watu hawahesabiwi ndoa ngapi wamepitia bali wanahesabiwa wamepitia vyuo vingapi hivyo ni jambo la kumshukuru Mungu.
Dida na Hezden

Dida na Ezden Jumanne.

Kabla ya kuvalishwa pete hivi karibuni, Dida aliwahi kuolewa na Juma Mchopanga ‘Mchops’, Gervas Mbwiga ‘G’ kabla ya kuolewa na mtangazaji mwenzake, Ezden Jumanne Ntambi ambaye walishindwana na kusababisha ndoa hiyo kuvunjika kutokana na migogoro ya mara kwa mara.

Leave A Reply