The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kutokuelewana kwa Miaka Miaka Kadhaa, Hatimaye Diamond, Baba’ke Wapatana

diamond-2 STORI: GLADNESS MALLYA NA MUSA MATEJA | Gaztei la Risasi Jumamosi, Toleo la Desemba 24, 2016

DAR ES SALAAM: Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha katika dunia hii ya duara! Baada ya kutofautiana kwa muda mrefu na baba yake, mzee Abdul Jumaa, hatimaye staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’, amepatana na mzazi wake huyo.

Habari za uhakika kutoka kwenye chanzo cha kuamini­ka katika familia ya Diamond zilieleza kuwa, hivi karibuni staa huyo na baba yake waliamua kupotezea maneno ya watu na kwamba wafanye wafanyavyo ku­hakikishia kuwa wanamaliza to­fauti zao hivyo kwa sasa wanaju­liana hali kama baba na mtoto au mtoto na baba na kushirikishana katika mambo yao.

“Unajua kati ya vitu alivyokuwa akivitamani Diamond ni kuwa vi­zuri na mzee (baba Diamond) na hicho ndicho kilichofanyika.

“Kizuri zaidi ni kwamba, baba Diamond amekuwa akimuomba Diamond msamaha na kujutia kosa lake (kumtelekeza na mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ tangu akiwa mdogo) kwa hiyo Diamond akaona bora amsame­he na kusahau yaliyopita kwani si ndwele badala yake wagange

 mapya.

baba-diamond-1 Baba Diamond

AANZA KUMTUMIA HELA

“Kwanza katika kuthibitisha kwamba wapo vizuri, Diamond alianza kwa kumjulia hali baba yake hasa juu ya kuumwa kwake kisha kumtumia hela ndogondogo za matumizi to­fauti na zamani maana katika kuomba msamaha, baba Dia­mond alimuomba sana amsai­die kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa miguu na hali ya kimaisha kuwa si nzuri kiivyo.

“Mbali na hivyo, pia am­emuwekea utaratibu wa kumpa mtonyo kila mwezi ili naye afaidi matunda ya mwanaye.

“Kinachoonekana kila mmoja aligundua kosa lake au aliwekwa chini na kuku­baliana kabisa kwamba mwenendo wa mgogoro kati ya baba na mtoto au mtoto na baba hauta­waacha sala­ma.

diamond-1“Kuna wal­iosema ki­tendo cha Diamond kumtenga baba yake ki­likuwa kinam­peleka kwenye laana lakini wen­gine walisema manung’uniko yake kuwa baba yake alimtele­keza nayo yasingemuacha baba Diamond salama hivyo kupa­tana kwao ni jambo kubwa mno kwenye maisha yao na hata mashabiki wa Chibu (Diamond) watafurahi kwamba kwa sasa yupo vizuri na mshua wake,” kilifunguka chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini hata kwa mtutu wa bunduki.

baba-diamond-2HUYU HAPA BABA D

Baada ya kuinyaka ishu hiyo,

 gazeti hili lilianza kwa kumsaka baba Diamond ambaye alipopa­tikana nyumbani kwake, Mago­meni-Kagera jijini Dar alithibi­tisha kupatana na mwanaye huyo na kwamba muda mfupi baadaye alimwambia mwandi­shi wetu kuwa ana safari ya kwenda nyumbani kwa Dia­mond, Madale-Tegeta, Dar.

“Watu wanaposema kuwa Diamond hanisaidii kwa sasa hivi hawajui ukweli. Ukweli ni kwamba mimi ananisaidia na hatuna tatizo lolote.

“Kwanza hapa nina safari ya kwenda Madale kwa hiyo kama una nafasi twende wote,” al­isema baba Diamond akionesha sura ya nuru na bashasha.

baba-diamond-3HADI MADALE

Hata hivyo, kama alivyoomba, mwandishi wetu aliambatana na baba Diamond hadi Madale na kushuhudia akitinga ndani huku mwandishi wetu akiishia getini baada ya kuzuiwa na walinzi.

Akiwa nje ya nyumba hiyo, mwandishi wetu alimshuhudia baba Diamond akiwa kwenye pilika mbalimbali akiingia na kutoka kwenye nyumba hiyo akionekana mwenye uzoefu maeneo hayo kutokana na namna alivyokuwa akisalimi­ana na majirani.

Uchunguzi wa gazeti hili, ulibaini kuwa wakati baba Diamond akijiachia kwa mwa­naye huyo, wenyeji wake hasa mwanaye Diamond, mama Diamond na mkwewe Zari­nah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ hawakuwepo.

DIAMOND AJIBU KWA KIFUPI

Gazeti hili lilipomtafuta Diamond na kumuuliza juu ya suala hilo alijibu kwa kifupi: “Mimi na mzee tupo fresh tu hamna tatizo.”

mama-dMamam Diamond

MAMA DIAMOND VIPI?

Kwa upande wake mama Dia­mond hakupatikana nyumbani kwake, Tandale wala Madale kwa maelezo kuwa yupo nchini Af­rika Kusini akimlea mjukuu wake mpya lakini huko nyuma aliwahi kukaririwa na gazeti hili akizun­gumzia mtafaruku wa Diamond na baba yake:

“Huwa ninaumia kwani Dia­mond kila mwezi huwa anapeleka hela ya matumizi kwa baba yake, sasa sijui maneno kuwa wana ugomvi yanatoka wapi? Ninacho­jua kwa sasa hawana shida ka­bisa na mambo ni poa.”

front-risasi

Gaztei la Risasi Jumamosi, Toleo la Desemba 24, 2016

HUKO NYUMA

Diamond na baba yake wame­kuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu ambapo mzazi huyo alikuwa akilalamika kwamba mwanaye huyo hakuwa akimjali na hata alipokuwa akijaribu kum­pigia simu alikuwa hampi ushiri­kiano.

Kwa upande wake Diamond amekuwa beneti na mama yake kwa madai kuwa baba yake huyo alimtelekeza baada ya kuten­gana na mama yake kisha akaoa mwanamke mwingine lakini sasa ‘mambo ni kama Ulaya mwanan­gu’.

ILIKUPITA HII?

Mpaka Home; Haya Ndo’ Maisha Halisi ya Darassa, Cheki Video Akipika Msosi Gheto

Comments are closed.