The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kuzidiwa na Corona, Marekani Yaiangukia China

0

BAADA ya kurushiana maneno kwa muda mrefu, kila mmoja akimshutumu mwenzake kwamba ameleta janga la virusi vya corona, hatimaye serikali ya Marekani na China zimeamua kukaa meza moja na kuomba kushirikiana ili kuudhibiti maambukizi ya virusihivyo yanayosababisha ugonjwa wa Covid -19.

 

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Rais wa Marekani, Donald Trump, leo Machi 27, 2020, ameandika; “Nimemaliza kufanya mazungumzo mazuri na Rais wa China, Xi Jinping. Tumezungumza kwa kina kuhusu madhara makubwa yanayosababishwa na CoronaVirus katika sehemu kubwa ya dunia yetu. China imepitia hali hii kwa ugumu na imejenga uelewa mkubwa kuhusu virusi hivi. Tutafanya kazi kwa karibu na pamoja. Heshima kubwa kwao!”

Ikumbukwe kuwa mpaka sasa Marekani ndiyo inaongoza kwa kuwa na watu wengi walioambukizwa CoronaVirus.

Marekani: wagonjwa 85,604
China: wagonjwa 81,340
Italy: wagonjwa 80,589.

 

 

 

Leave A Reply