The House of Favourite Newspapers

Baada ya Ndoa, Mwanaheri Afunguka Kuachana na Filamu

LICHA ya madai kwamba amepigwa stop kuendelea kucheza filamu na mumewe, Khamis baada ya kuolewa hivi karibuni, mrembo wa filamu za Kibongo, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ ameibuka na kueleza ukweli.

Za Motomoto News ilizungumza na Mwana ambaye alifunguka kuwa, amekuwa akiyasikia madai hayo, lakini ukweli ni kwamba hata iweje, kamwe hawezi kuachana na kazi yake ya filamu kwani ni fani anayoipenda licha ya kuwa ana elimu kubwa, lakini aliachana na kuajiriwa na kufanya kile alichokuwa anakipenda na mumewe anaheshimu hilo.

“Mume wangu anaiheshimu na anaipenda sana kazi yangu hivyo hawezi kunizuia kuigiza, bado ninaendelea na sanaa kama kawaida maana ndoa hainizuii chochote,” alisema Mwana.

Comments are closed.