The House of Favourite Newspapers

Lechantre: Wamebaki Singida United, Ninayo Dawa Yao

Kocha wa Simba, Pierre Lechantre (kushoto) akiongea na Jonas Mkude.

BAADA ya kuvuna pointi tatu kwa watani wao wa jadi Yanga, Kocha wa Simba, Pierre Lechantre amesema amebakiza mechi moja pekee ngumu ambayo ni dhidi ya Singida United, amesema anayo dawa yao.

 

Lechantre raia wa Ufaransa ametoa kauli hiyo baada ya Simba kuifunga Yanga bao 1-0 wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mfungaji akiwa ni Erasto Nyoni.

Kikosi cha Simba.

Simba yenye pointi 62 kileleni mwa Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuvaana na Singida United Mei 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Namfua, mjini Singida katika muendelezo wa ligi hiyo.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Lechantre alisema anaijua vizuri Singida United kwani aliiona kwenye mechi ya ligi kuu ikicheza dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

“Ukizizungumzia timu bora katika ligi msimu huu ni lazima utaitaja Singida United ambayo imesa­jili wachezaji wengi bora kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Uganda na Rwanda.

 

“Hivyo, siyo nyepesi ni lazima nifanye maandalizi ya kutosha kuhakikisha ninaifun­ga Singida ili nijihakikishie ubingwa wa ligi katika msimu huu tunaowania na Yanga.

 

“Nashukuru tayari nimefanya kikao na wachezaji wangu na kuzungumza mambo kadhaa ikiwemo ya mikakati ya ubingwa ambayo tayari tumeikamilisha ikiwemo hili la kushinda mechi moja na kutoa sare moja, kwani ili tuwe mabingwa tunahitaji pointi nne pekee,” alisema Lechantre.

 

Katika mchezo uliopita, Simba iliifunga Singida United mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Comments are closed.