The House of Favourite Newspapers

Baba Ampa Mimba Mwanae wa Kumzaa, Alishampa Mwingine – Video

0

WASWAHILI wanasema ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni! Hebu vuta picha kichwani mwako, baba mzazi anafanya mapenzi kwa nguvu na mwanaye wa kumzaa, na kama hiyo haitoshi, anampa ujauzito kabisa! Ni jambo lisilowezekana si ndiyo? Haingii akilini si ndiyo?

 

Sasa kwa taarifa yako, tukio kama hilo limetokea Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani ambapo mwanaume anayetambulika kwa jina la Fadhil Mshamu anatuhumiwa kumuingilia kimwili mwanaye wa kumzaa ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu maalum, kisha kumpatia ujauzito.

 

Mbaya zaidi, binti huyu aliyefanyiwa ukatili huo, ana matatizo ya mtindio wa ubongo! Ama kwa hakika dunia haina huruma! Mpaka sasa binti huyo ana ujauzito wa miezi miwili, ujauzito aliopewa na baba yake mzazi.

 

Timu ya waandishi mahiri wa habari za uchunguzi na za kijamii kutoka Global TV, ikiongozwa na Richard Bukos na Issa Mnally, imefunga safari mguu kwa mguu mpaka eneo la tukio, Kibaha Kwa Mfipa mkoani Pwani kwenda kuchimba kwa undani kuhusu tukio hili. Mwamvua Ally John, ni mama wa binti aliyepewa ujauzito na hapa anaeleza jinsi alivyogundua suala hilo.

 

Leave A Reply