The House of Favourite Newspapers

Baba: Msuva Anakwenda Hispania

1
Mchezaji wa Difaa Al Jadida ya Morocco, Somon Msuva.

BABA wa winga wa zamani wa Yanga, Happygod Msuva ambaye ni Simon ameibuka na kuwaambia Simba kuwa kama walishindwa kumsajili mchezaji huyo akiwa hapa nchini, basi wasahau akiwa Morocco.

Kauli hiyo ameitia juzi Jumatano ikiwa ni siku chache tangu Msuva ajiunge na Klabu ya Difaa Al Jadida ya Morocco ambapo tayari ameichezea mechi moja na kufunga bao moja.

Winga huyo alijiunga na klabu hiyo baada ya uongozi wa Yanga kukubali kumuuza akiwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea timu hiyo.

Akizungumza na Spoti Hausi inayorushwa na Global TV Online, Happygod alisema Simba walikuwa wanamuwania Simon muda mrefu kabla na baada ya kutua Yanga, lakini walishindwana kuanzia alipokuwa akiichezea Moro United.

Happygod alisema kwa mwanaye alipofikia hivi sasa katika soka anafikiria kucheza soka la kimataifa zaidi kwenye nchi za Hispania na siyo kurejea Tanzania.

Aliongeza kuwa anaamini mwanaye atafanikisha ndoto zake hizo kutokana na ndoto zake alizozipanga zilizoanza kufanikiwa tangu akiwa utotoni.

“Kwa hatua ya soka aliyofikia mwanangu siyo mchezaji wa kurudi kuichezea Simba ambayo ilikuwa inamuwania siku za hivi karibuni akiwa Yanga.

“Simba kama kumsajili basi wangemsajili kipindi ambacho Rage (Ismail) na Kaburu (Geofrey Nyange) walipokuwa madarakani nilipompeleka Msuva akiwa Moro Utd kwao lakini hawakumpokea,” alisema Happygod.

Stori: Wilbert Molandi | Championi Ijumaa

 

1 Comment
  1. […] wa familia hiyo akaanza kumnyanyapaa kwa kumpiga na kumtenga na watoto wengine. “Niliumia sana. Baba badala ya kumsaidia mama, akaanza […]

Leave A Reply