The House of Favourite Newspapers

Baba P… Baba Pili… Baba Pilima!-9

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA:
Ghafla, baba Pilima akatokea kutoka chumbani akiwa ndani ya nguo za kulalia…
“Mbona kama nasikia mimi nimempigia simu mama Pilima wakati sijashika simu yangu tangu kumekucha. Au sijasikia sawasawa?” alihoji baba Pilima huku akipiga miayo.
JIACHIE MWENYEWE…

“Nilidhani umepiga kwenye simu ya wifi,” alisema dada yake huyo.
Baba Pilima aliporudi chumbani, mama Pilima alikaa sebuleni na wifi yake, wifi akaanza kusema…

“Wifi, huyo uliyemsevu kwa jina la baba Pilima kwenye simu yako ni nani? Maana simu ilipoita nikajua ni kaka, ndiyo maana nikakwambia kaka anapiga. Lakini pia nilishangaa kwa nini kaka apige wakati yumo humuhumu ndani?”

“Wifi yule anaitwa mama Sakina, anakaa mtaa wa mwisho kule. Siku namsevu sijui ilikuaje, nikaandika jina la kaka yako, lakini sikulifuta, tena ngoja nimpigie,” alisema mama Pilima huku akishika simu, akaiweka sikioni, baada ya muda akaongea…
“Ee mama Sakina…naona ulinipigia…aaa! oke…sawasawa…saa ngapi…oke sawa,” akakata simu na kumgeukia wifi yake…

“Kumbe alitaka niende nyumbani kwake, ana vitenge vizuri kutoka Zaire,” alisema mama Pilima. Lakini ukweli ni kwamba, hakupiga simu kwa mtu yeyote yule, achilia mbali mama Sakina…

“Oke, na siku ile ulipiga simu ikasomeka jina la baba Pili naye ni nani wifi?” wifi mtu huyo aliuliza tena.

Mama Pilima alianza kuhisi wifi yake huyo ana lake moyoni…
“Haiwezekani aniulize maswali kama yeye ndiyo kanioa?” alijisemea moyoni…
“Wifi, mbona unanichunga sana, kwani nimekufanyia kosa gani? Unaniuliza maswali kama wewe ndiyo baba Pilima bwana…aaah! wifi haifai hivyo,” alilalamika mama Pilima.

Ilibidi wifi yake awe mpole…
“Basi yaishe wifi.”
Lakini moyoni, wifi mtu huyo alikuwa ana maswali kibao kuhusu majina yale, hakukubali kama baba Pilima ni mama Sakina. Pia alitia shaka kwa baba Pili…
“Huyu wifi ameanza michepuko,” alisema moyoni wifi mtu huyo.

Walikwenda kanisani, walisali, wakatoka kurudi nyumbani. Wakiwa njiani, mama Pilima alipokea simu, wifi yake akawa makini kumsikiliza…
“Eee…mzima sijui wewe..? Hawajambo akina Pilima..?” hii hawajambo akina Pilima, wifi mtu huyo alijisahau, akashtuka sana na kukata simu kisha akatuma meseji…
“Tuchati, niko na wifi yangu.”

Wifi naye alishtuka kusikia ‘hawajambo akina Pilima’…
“Kumbe..! Kumbe kuna mtu anaitwa baba Pilima. Ndiyo nimejua sasa,” alisema moyoni wifi huyo.

“Nilitaka kujua kama leo unaweza kuwa free kidogo,” aliuliza baba Pilima feki.
“Natoka kanisani. Labda baadaye. Ulitakaje kwani?”
“Nilitaka tuonane mahali…”

“Kuonana kwa kuzungumza au zaidi ya kuzungumza?”
“Zaidi ya kuzungumza.”
“Mh! Baba Pilima bwana. Nitaachika mwenzako ujue.”
“Hamna bwana! Nimekumisi sana ujue. Da!”

“Mmh! Si jana tu tulikuwa wote my darling?”
“Si ndiyo maana ya kukumisi jamani! Hata kama tulikuwa wote lakini kila nikikukumbuka bado napenda tuwe wote.”
Mama Pilima alijikuta akiachia tabasamu la ndani kwa ndani ili wifi yake asijue.
“Basi mchanamchana nitakwambia.”
“Poapoa baby wangu.”

Baada ya muda, meseji iliingia kwenye simu ya mama Pilima ikiwa inatokea kwa baba Pili sasa…
“Upo?”

Mama Pilima baada ya kuisoma, hakuona sababu ya kutomjibu kama ilivyokuwa siku kadhaa nyuma…
“Nipo…wewe je?”
“Mimi nipo, hatuonani?”

“Ubize kidogo, lakini tutaonana tu, usijali,” alijibu mama Pilima huku moyoni akisema…
“Tatizo si kuonana, bali umeshawahiwa na mwenzako baba Pilima.”
***
Saa kumi jioni, mama Pilima alijipara tayari kwa kutoka. Ni baada ya mumewe kuondoka. Akabaki wifi mtu bado akiwa na mawazo kibao kuhusu mama Pilima.
Alipotoka tu mama Pilima, alimtumia meseji baba Pilima feki…
“Mimi ndiyo natoka nyumbani sasa, tunakutana wapi?”
“Njoo mpaka pale pa jana.”
“Oke.”

Mama Pilima alitembea hadi kituoni ili kuchukua Bajaj. Lakini ile anafika tu, gari dogo jeupe lilisimama mbele yake na kupiga honi mfululizo. Vioo vilikuwa na tinted kwa hiyo hakumwona dereva ndani.

Honi iliendelea kupigwa kisha kioo cha upande wa abiria kikafunguliwa nusu, dereva akaongea na mtu mmoja aliyesimama kituoni hapo akisubiri usafiri wa daladala. Kisha yule mtu akamgeukia mama Pilima aliyekuwa amesimama pembeni…

“Anti unaitwa kwenye gari,” alisema yule abiria.
“Na nani?”
“Eti anakuuliza wewe nani?” aliuliza yule abiria akiwa ameinama kidogo ili amuone vizuri yule abiria…

“Anasema anaitwa baba Pili,” yule abiria alimwambia mama Pilima.
Mama Pilima akatembea kwa kasi hadi mlangoni mwa gari…
“Mzima baba Pili?”
“Mzima, twende nikupe lifti.”

Je, unajua nini kilitokea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, siku ya Jumatatu.

Leave A Reply