The House of Favourite Newspapers

Baba wa KR Mullah Afariki Dunia

0

MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini Rashid Ziada ‘KR Mullah’ amefiwa na baba yake mzazi mkoani Lindi.

 

Taarifa ya kifo cha mzazi wa msanii huyo, kimeelezwa na msanii mwingine wa muziki wa kizazi kipya, Amani Temba ‘Mheshimiwa Temba’, kupitia ukurasa wake wa instagram leo.

 

“Pole sana KR Mullah TMK kwa kuondokewa na baba yako mzazi, Mzee Ziada, hakika kazi ya Mungu haina makosa,” ameandika Mheshimiwa Temba, ambaye pamoja na KR Mullah walitamba na kundi la TMK Wanaume Familiy.

 

Kwa mujibu wa Temba, msiba huo ulitokea usiku wa kuamkia leo mkoani Lindi na kuwa taratibu nyingine za mazishi zitatolewa leo.

Leave A Reply