The House of Favourite Newspapers

Baby Madaha: Acheni Bifu Za Kisiasa

0

Madaha1.jpgStaa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha.

Gladness Mallya

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha amewataka wasanii wenzake wenye bifu za kisiasa kuachana nazo kwani kuna maisha baada ya uchaguzi.

“Inawezekana wanagombana kwa ushabiki wa vyama kwa sababu hawajui maana ya siasa na itikadi, watu wengi wanashindwa kutofautisha hayo mambo, matokeo yake ni bifu zisizo za msingi,” alisema nyota huyo baada ya kuombwa maoni yake kuhusu ishu hiyo.

Wakati nchi ikijiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa urais, ubunge na udiwani, mastaa mbalimbali wamejikuta wakiingia kwenye bifu kwa kutoleana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutofautiana kiitikadi kama ilivyotokea hivi karibuni kwa Jacqueline Walper ‘Wolper’ na Aunt Ezekiel.

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS UPATE HABARI KEMKEM ZA UCHAGUZI MKUU

globalbreakingnews.JPG

Leave A Reply