The House of Favourite Newspapers

Bado Menina Ana Kinyongo na Mwijaku

0

MWANAMAMA anayefanya kila kitu kuanzia usanii wa muziki wa Bongo Fleva, uigizaji wa Bongo Movies, u-MC wa sherehe mbalimbali na vinginevyo, Menina Attick amejikuta akishindwa kujizuia kutokwa na machozi huku akionesha dhahiri bado ana kinyingo na Mwijaku.

Menina alijikuta katika hali hiyo alipokuwa akieleza changamoto anazopitia kwa sasa baada ya kupata msiba wa kuondokewa na mume na mtoto wake.

Menina; kila anapohojiwa haachi kumtaja Mwijaku kama mtu aliyemuumiza katika maisha yake.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply