The House of Favourite Newspapers

Bahati Nasibu Shinda Nyumba… Siku 8 Zijazo, Mshindi Mjengoni

0

WAKATI washindi watatu waliopatikana katika droo kubwa ya Shinda nyumba wakipewa zawadi zao Jumatano iliyopita, mshindi wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, George Majaba, siku nane zijazo atakabidhiwa mjengo wake uliopo Bunju B, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Majaba, ambaye ni kondakta wa mabasi ya abiria yanayofanya safari zake kati ya Dodoma na Dodoma vijijini, alishinda wakati wa droo hiyo iliyochezwa Septembe 27 mwaka huu katika viwanja vya Las Vegas, vilivyopo Mabibo na hivyo kuhitimisha zoezi hilo lililodumu kwa miezi sita.

Majaba anatarajiwa kukabidhiwa nyumba hiyo katika hafla fupi itakayofanyika Oktoba 31 mwaka huu, itakayoanzia katika ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori na baadaye katika eneo la tukio huko Bunju.

“Tunataka kufanya kitu kidogo tofauti na cha kumtia faraja mshindi wetu, kwa maana hiyo tumeandaa mapokezi maalum, tumeandaa pikipiki na magari ambayo yatampokea Ubungo Terminal na kuja naye hadi ofisini kwetu (Zilizopo Sinza Mori, zamani Johanesburg Hotel).

“Pale kutakuwa na utambulisho rasmi wa mshindi wetu ikiwa ni pamoja na kufanya mahojiano na vyombo vya habari na kisha tutaanza safari ya kuelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumkabidhi nyumba yake,” alisema Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.

“Tumeamua kumpa nyumba ikiwa kamili kabisa, atakachofanya yeye ni kuja na begi lake na kuanza maisha, hiyo yote ni kuonyesha jinsi gani Global Publishers imedhamiria kubadili maisha ya wasomaji wake, pamoja na thamani kubwa ya nyumba, lakini tumeona tumuongezee na nishati hii muhimu ili kumpunguzia jukumu la kuhangaika kuingiza umeme,” alisema Mrisho.

Hii ni mara ya pili kwa Global Publishers, kampuni pekee ya uchapaji magazeti katika historia, kuwahi kutoa zawadi ya nyumba kwa wasomaji wake.

Kabla ya kupatikana kwa mshindi wa awamu hii ya pili, bahati nasibu hiyo ilifanya droo ndogo tano katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, ambako wasomaji zaidi ya 30 walijipatia zawadi kemkem, zikiwemo pikipiki, ving’amuzi, televisheni flat screen, simu za kisasa za mikononi, kofia na fulana.

 Stori: Mwandishi Wetu, Ijumaa WIKIENDA

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android Bofya ===> Google Play

iOS Bofya ===>Apple Store

LULU MAHAKAMANI: Kanumba Alinikimbiza na Panga!

Leave A Reply