The House of Favourite Newspapers

Balama: Huyu mtu hapa Yanga ni kiboko

KIUNGO mpya wa Yanga, Balama Mapinduzi ameonekana kushangazwa na namna ambavyo Kocha Mwinyi Zahera anawanoa. Balama alijiunga na Yanga hivi karibuni akitokea Alliance ya Mwanza, na alionyesha
kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa kirafiki wikiendi iliyopita.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Balama alisema kuwa japo amefundishwa na Zahera kwa siku chache tangu atoke mapumzikoni lakini ameanza kupata vitu tofauti ambavyo anaamini vitamsaidia kukuza kiwango chake.

“Zahera ni kocha mzuri sana kwa mimi amenifundisha siku chache lakini nimeanza kupata vitu vipya ambavyo naamini vitanisaidia katika kukuza kiwango changu,” alisema Balama.

 

Yanga kwa sasa ipo visiwani Zanzibar kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Mlandege na Malindi FC ikiwa sehemu ya maandalizi ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Township Rollers Agosti 10.

Comments are closed.