The House of Favourite Newspapers

Balama, Nchimbi Wamuingiza Kocha Wao Mtegoni

0

KIUNGO Balama Mapinduzi na straika Ditram Nchimbi, wamepewa majukumu mapya na kocha wao, Luc Eymael ya kuhakikisha wanatumia vizuri uwezo wao wa kukimbia na mipira kutengeneza nafasi za kufunga kwa wenzao kutokana na kikosi hicho kuwa na wastani wa kupata mabao machache kwenye mechi.

 

Kocha huyo amefunguka kuwa anawataka wachezaji hao kwa kushirikiana na Deus Kaseke, Mrisho Ngassa na Yikpe Gislein ambao wana uwezo wa kukimbia ndiyo wawe watengenezaji wakubwa wa mabao ya kikosi hicho.

 

Eymael amepata akili hiyo baada ya kuona kuna ugumu wa kufunga mabao kwa kupitia katikati ya eneo la wapinzani wao ambao wanacheza kwa umakini kulilinda eneo hilo.

Kocha huyo ameliambia Championi Jumatano, kuwa amebaini kutumia wachezaji hao wenye kasi ndiyo itakuwa silaha tosha kwa washambuliaji wake kufunga kirahisi kama ambavyo ilivyokuwa kwenye mechi yao na Mtibwa Sugar, Jumapili iliyopita.

 

“Unajua kwenye mechi na Mtibwa Sugar nilibaini kuwa wapinzani wangu wanatumia vizuri eneo lao la kati katika kujilinda na hawatoi nafasi ya kupita hapo.

 

“Ndipo nilipomuingiza Nchimbi kwa sababu najua ana uwezo wa kukimbia pembeni kwa ajili ya kutengeneza nafasi na kweli jambo hilo likatimia.

 

“Ninataka kutumia wachezaji wenye spidi zaidi ili tufunge mabao. Nitawatumia Balama, Yikpe, Ngassa, Kaseke na Nchimbi ambao wana spidi kulifanya suala hilo,” alieleza Mbelgiji huyo.

Leave A Reply