The House of Favourite Newspapers

Balozi Dk. Nchimbi, Ashiriki Kikao cha Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu Mkoa wa Njombe

0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, akiwa kwenye Kikao cha Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Njombe, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Njombe, Njombe Mjini, kabla ya kuelekea kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa Mkoa wa Njombe, leo asubuhi, Aprili 19, 2024.
Dk Nchimbi, akiambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Oganaizesheni, Ndugu Issa Haji Usi Gavu na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makala, yuko mkoani Njombe kwa ziara ya siku mbili, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika mikoa 6 ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.
Leave A Reply