The House of Favourite Newspapers

Balozi Dkt. Nchimbi Awatembelea Waathirika wa Mapolomoko Mlima Kawetele, Mbeya

0

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akimkabidhi mmoja wa waathirika na maporomoko fedha Tsh. Mil 10 kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wote wa maporomoko ya Mlima Itezi Mkoani Mbeya leo Aprili 17,2023 wakati alipowatembelea katika kambi walipo shule ya Msingi Tambukareli.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Nchimbi, pamoja na msafara wake, leo Jumatano, Aprili 17, 2024, amewatembelea kuwajulia hali na kuwapatia pole wananchi wa Kata ya Itezi, Wilaya ya Mbeya Mjini, walioathiriwa na maporomoko ya Mlima Kawetele, hivi karibuni.
Mbali ya kuwasilisha salaam za pole za Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa waathirika hao wapatao 51, Dk Nchimbi, kwa niaba ya CCM, amewapatia pia pole ya fedha taslimu ya Sh. 10 milioni.
Wananchi hao ambao wamepewa makazi ya muda Shule ya Msingi Tambuka Reli, Mbeya Mjini, walishukuru pole na salaam hizo za Chama na Serikali, huku Dk. Nchimbi akiwasihi kuwa na subira wakati huu ambapo Serikali inaendelea kufanya tathmini ya kina juu ya tukio hilo ili kujua hatua stahiki za kuchukua kuzuia maafa zaidi.

 

Awali Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dk Emmanuel Nchimbi alitua Makao makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya na kufanya mkutano wa ndani wa kamati ya siasa kujua maendeleo ya Chama hicho kisha baada hapo Majira ya saa tisa atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja vya Luanda Nzovwe.

 

Leave A Reply