The House of Favourite Newspapers

Banda Awashangaza Wahariri Wa Championi na Spoti Xtra

Beki wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda (kulia) wakati akiwasili Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori. Kushoto ni Mwandishi wa Global, Said Ally.
Akipanda ngazi kuelekea ofisini
Akisalimiana na Mhariri wa Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula.
Banda akiongea jambo na Mhariri wa Championi Jumamosi, Elius Kambili.
Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph akimuonesha gazeti la Spoti Xtra Abdi Banda alipotembelea Ofisi za Global Group.
Banda akisalimiana na Mhariri wa Championi Jumatano,  Philip Nkini ofisini hapo.

BEKI wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda amewashangaza Wahariri wa Gazeti la Spoti Xtra na Championi baada ya kuonyesha utofauti mkubwa wakati ambao alikuwa anacheza soka nchini na sasa Afrika Kusini.

Beki huyo amesema kwamba soka la Afrika Kusini ni gumu na lenye changamoto nyingi huku timu zote 16 zikiwa na uwezo wa hali ya juu tofauti na hapa nchini ambapo kuna timu chache zenye nguvu na zinazoweza kufanya lolote kwenye soka.

(Picha: Sweetbert Lukonge | GPL)

Comments are closed.