The House of Favourite Newspapers

Banda Mambo Fresh Simba

Stori: Na Hadja Mgwai | CHAMPIONI | Dar es Salaam

ACHANA na uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza Simba, beki Abdi Banda ameshusha presha ya mashabiki wa timu hiyo kwa kusema yupo mbioni kusaini mkataba mpya wa miezi 18 kubaki klabuni hapo.

Mkataba wa sasa wa Banda umebakisha miezi mitatu tu ili ufikie tamati na sasa yupo katika mazungumzo na uongozi ili kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja na nusu.

Katika siku za hivi karibuni, uwezo wa Banda uwanjani umeonekana kuimarika kiasi cha kuisaidia Simba na kuonekana ameziba pengo la Juuko Murshid ambaye bado hajarejea kikosini.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Banda alisema anatarajia kuongeza mkataba wa mwaka na nusu klabuni hapo kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara baada ya ule wa sasa kuelekea kuisha.

“Natarajia kuongeza mkataba wa mwaka na nusu baada ya kumaliza mkataba wangu huu wa awali, kwa sasa tupo katika mazungumzo ya mwishomwisho na viongozi wangu kukamilisha suala hilo.

“Nadhani mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao (Machi) kila kitu kitakuwa kimekamilika, lakini kuhusu dau nitakalosaini siwezi kuliweka wazi kwa sasa ila mashabiki wajue nitaongeza mkataba,” alisema Banda.

Banda alisema anasikitika kukosa mechi ya leo dhidi ya Majimaji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea kwani anaamini angeweza kukisaidia kikosi chake. Banda anasumbuliwa na majeraha ya misuli.

Comments are closed.