The House of Favourite Newspapers

Banda Mikononi Mwa Mamelodi

0

BEKI Mtanzania anayecheza soka la kulipwa katika timu ya Highlands Park inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Abdi Banda, atakutana na Mamelodi Sundowns katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Kombe la NedBank.

 

Banda akiwa na kikosi chake, watakutana na Mamelodi Sundowns baada ya kuwatoa Kaizer Chiefs katika hatua ya 16 Bora kwa kuwafunga kwa penalti 5-4, mchezo uliopigwa Februari 22, mwaka huu kwenye Uwanja wa Makhukong. Muda wa kawaida matokeo yalikuwa sare ya 1-1.

 

Katika robo fainali, timu hizo zitaanzia nyumbani kwa Highlands Park Machi 14, mwaka huu, mchezo ukichezwa kwenye Uwanja wa Balfour Park.

 

Endapo Highlands Park  itapita hatua hiyo, Banda anaweza kukutana na timu yake ya zamani ya Baroka FC ambayo inanolewa na kocha wa zamani wa Simba, Dylan Kerr. Baroka robo fainali itacheza dhidi ya Black Leopards.

MASHABIKI YANGA WAKOSA IMANI NA KOCHA / “GOLI MOJA” UONGOZI Ufanye Maamuzi

Leave A Reply