The House of Favourite Newspapers

BARABARA MOSHI-DAR YAFUNGWA KWA MUDA KWA KUANGUKIWA NA MTI

Magari yakiwa yamesimama kusubiri sehemu ya mbele iliyokuwa imezibwa kutokana na mti mkubwa ulioanguka barabarani na kuziba njia nzima.

 

BARABARA ya Moshi-Dar imefungwa kwa muda asubuhi ya leo eneo la mbele ya  Chekereni karibu na daraja la Kileo karibu na Kifaru kutokana na kuanguka mti mkubwa katika barabara hiyo na hivyo kusababisha magari yashindwe kupita.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah, amesema mti mkubwa ulioanguka katika barabara hiyo ulisababisha magari yashindwe kupita na kusababisha foleni pande zote.  Vilevile, aliongeza kwamba, katika kugombania kupenya sehemu hiyo, magari mawili makubwa yaligongana katika kutaka kuukwepa mti huo na hivyo kuziba kabisa sehemu yote eneo hilo.

 

Hata hivyo, alisema, wakati hali hiyo ikiendelea, polisi walifika eneo hilo na kusaidiana na wananchi kuuondoa mti huo kwa kuukata na mapanga na baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, magari yaliendelea na safari zao kama kawaida.

 

Akizungumza na mtandao huu, Kamanda Issah, alisema si kweli kwamba barabara hiyo ilikuwa imefungwa tangu saa 6 za usiku mpaka muda huu, akisema hayo ni maneno ya uvumi na kwamba alichokisema na mtandao huu ndiyo hali halisi.

Comments are closed.