The House of Favourite Newspapers

Baraza La Wawakilishi Kupiga Kura Ya Kupeleka Mashtaka Ya Trump

0

Baraza linatarajiwa kupiga kura leo Jumatano 15, 2019 ili kupeleka mashtaka dhidi ya Rais Trump mbele ya Bunge la Seneti ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kuanza kwa kesi ya kumuondoa madarakani

 

Spika wa Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na chama cha Democratic na mpinzani mkuu wa Donald Trump katika baraza hilo, Nancy Pelosi, alitangaza Jumanne wiki hii baada ya mkutano faragha na wabunge kwamba mashtaka yanayomkabili Donald Trump yatapelekwa mbele ya Bunge la Seneti leo Jumatano Januari 15.

 

Bunge la seneti linadhibitiwa na chama cha Republican cha Donald Trump. Wadadisi wanasema ni vigumu bunge hilo lipitishe mashitaka hayo ya rais kutoka chama kinachodhibiti taasisi hiyo kubwa nchini Marekani.

 

Donald Trump anakabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia Bunge kufanya shughuli zake.

 

Upinzani unaamini kwamba Rais Donald Trump alitumia rasilimali za serikali kushinikiza Ukraine kuchunguza mgombea urais kutoka chama cha Democratic Joe Biden, mpinzani wake katika uchaguzi wa urais wa Novemba. Upinzani unamshtumu

Leave A Reply