The House of Favourite Newspapers

Barcelona Yabanwa na Real Madrid Nyumbani – Video

0

TIMU ya Barcelona imebanwa na Real Madrid usiku wa kuamkia leo, Desemba 19, 2019, baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Nou Camp.

 

Matokeo hayo yamezidisha msisimo wa kuwania ubingwa wa ligi kuu hiyo msimu huu kwa kuwa timu hizo zimeendelea kulingana pointi 36, lakini Barcelona iko kileleni kwa uwiano mzuri wa idadi ya mabao.

Wakati huohuo, idadi kubwa ya mashabiki wa Barcelona walikamatwa jirani na uwanja huo kutokana na vitendo vya kuandama kisiasa.

Awali, mchezo huo ulipangwa kuchezwa Oktoba 26 kabla ya kuahirishwa kutokana na hali ya kisiasa iliyopo katika Jimbo la Katalunya inapotoka Barcelona wanaotaka kujitenga.

Barcelona: Ter Stegen; Semedo (Vidal, min. 55), Pique, Lenglet, Jordi Alba; Busquets, De Jong, Sergi Roberto; Griezmann (Ansu Fati, min. 83), Luis Suarez, Messi

Real Madrid: Courtois; Carvajal, Sergio Ramos, Varane, Mendy; Casemiro, Kroos, Valverde (Modric, min. 80), Isco (Rodrygo, min. 80); Bale, Benzema

Magoli: Hakuna

Referee: Hernandez Hernandez (Las Palmas).

Yellow Cards: Rakitic (Min. 21) for Barcelona, Suarez (Min. 40) for Barcelona, Lenglet (Min. 45) for Barcelona, Casemiro (Min. 66) for Real Madrid, Bale (Min. 70) for Real Madrid, Isco (Min. 76) for Real Madrid, Ramos (Min. 78) for Real Madrid, Carvajal (Min. 92) for Real Madrid

Red cards: None

Stadium: Camp Nou

Attendance: 93.426

Leave A Reply